MPYA: WATANO WAKAMATWA TUKIO LA UGAIDI KENYA!!!,WAMO PIA.....
Serikali ya Kenya inasema kuwa watu watano wanazuiliwa kufuatia
shambulizi lililondeshwa na kundi la Al shabaab kwenye chuo kikuu cha
Garissa ambapo karibu watu 150 waliuawa.
Baadhi ya washukiwa hao walikamatwa wakijaribu kutorokea taifa jirani la Somalia,waziri wa usalama nchini Kenya amesema.
Mwanafunzi wa kike ambaye aliponea shambulizi hilo ambaye alipatikana
amejificha saa 48 baada ya shambulizi hilo kwa sasa anahudumia na
shirika la msalaba mwekundu.
Takriban watu 148 wengi wao wakiwa wanafunzi waliuawa wakati wapiganaji walipovamia chuo kikuu cha Garissa.
Kundi la Alshabaab kufikia sasa limeapa kutekeleza ,mashambulizi mabaya dhidi ya Kenya.
Kundi hilo linasema kuwa vitendo vyake ni vya kulipiza kisasi vitendo
vinavyofanywa na jeshi la kenya dhidi ya kundi la Alshabaab nchini
Somalia.
Alshabaab pia lililaumiwa na shambulizi la West Gate mjini Nairobi nchini Kenya mwaka 2013 ambapo watu 67 waliuawa.
Tayari maafisa wa polisi katika taifa jirani la Uganda wanasema
wamepokea habari zinazosema kwamba shambulizi kama hilo linapangwa
nchini humo
No comments:
Post a Comment