KWA
wiki moja sasa, baadhi ya vyombo vya habari vimekuwa vikiripoti kwamba,
kujisikia kizunguzungu hatimaye kuanguka na kupoteza fahamu
kulikomtokea Mchungaji wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima
wakati akihojiwa na polisi kulitokana na kuulizwa maswali yaliyohusu
namna alivyozipata mali zake, Risasi Jumamosi linakupa zaidi.
Mchungaji wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima.
Machi 28, mwaka huu Mchungaji Gwajima alipojisalimisha Kituo Kikuu cha
Polisi Kanda Maaalum ya Dar es Salaam kwa madai ya kumtolea maneno yenye
kuudhi Askofu wa Kanisa la Romani Katoliki Jimbo Kuu la Dar, Mwadhama
Polycarp Kadinali Pengo, alijikuta akizidiwa ghafla na kukimbizwa
Hospitali ya TMJ kwa matibabu huku akiwa amepoteza fahamu.
Ilidaiwa kuwa, Gwajima alipokwenda kituoni hapo kujisalimisha alitarajia
kukutana na mahojiano ya kuhusu kauli yake ya kumkashifu Kadinali
Pengo, lakini matokeo yake akakumbana na maswali ya kuhusu mali zake.
WALIVYOSEMA WATU
“Unajua
Gwajima yeye alipoambiwa ajisalimishe Central kwa kumkashifu Pengo
alijua akifika pale ataulizwa kwa nini ulimtusi Pengo? Alikukosea nini?
Huoni kama yule ni mtu mzima kuliko wewe? Je, uko tayari kumwomba radhi?
Lakini matokeo yake katikati ya maswali akaulizwa mali alizonazo
alizipata kwa njia gani?”
KWA NINI ALIZIMIA SASA?
Gari lake la kifahari.
“Sasa suala siyo kwamba swali hilo la kuhusu mali lilikuwa na shida
kwake, bali lilikuwa la ghafla ndiyo maana akajikuta akichanganyikiwa na
kupoteza fahamu,” kilisema chanzo kimoja.“Wengi wanasema alipoulizwa
kuhusu mali alizimia kwa sababu mali zenyewe si halali, hapana! Zile
mali ni halali kabisa ila swali halikuwa kwenye mawazo ya Gwajima,”
kiliendelea kusema chanzo.
RISASI JUMAMOSI LAZICHIMBA
Kufuatia
madai hayo, Risasi Jumamosi liliamua kuzama kazini na kuzichimba mali
hizo kwa nia ya kuzitambua ambapo uchunguzi wa kina uliofanywa ulibaini
kwamba, Mchungaji Gwajima anamiliki gari la kifahari aina ya Hummer 2
ambalo gharama ya manunuzi mpaka kufika Tanzania ni wastani wa shilingi
milioni 250.
Mbali
na gari hilo la kifahari, Gwajima amewanunulia wachungaji wake 30
magari ya kutembelea ili kupambana na tatizo la usafiri jijini Dar.
Nyumba yake ya kifahari.
MAGARI YAANIKWA
Baadhi
ya magari hayo ni Subaru Forester (sokoni linauzwa shilingi milioni
17), Mitsubishi Pajero (shilingi milioni 16), Toyota Spacio new model
(milioni 20) na Toyota Harrier Lexus (milioni 35).
MJENGO WA MAANA
Risasi
Jumamosi lilibaini pia kuwa, mchungaji huyo anaishi kwenye nyumba yake
ya kifahari ya ghorofa nne iliyopo Mbezi Beach, jijini Dar es Salaam.
Helkopta yake.
MABASI 20
Kweli
Gwajima ni tajiri kwani Risasi Jumamosi likabaini kuwa, pia anamiliki
mabasi 20 ambayo ni kwa ajili ya kuwabeba waumini wa kanisa lake wakati
wa kwenda kwenye ibada na kurudi makwao katika sehemu mbalimbali za Jiji
la Dar. Mabasi hayo kila moja alilinunua kwa shilingi milioni mia moja
na ishirini.
PIA KUNA HELKOPTA
Pia,
miezi ya hivi karibuni, Gwajima alinunua helkopta (chopa) kwa ajili ya
kuzungukia sehemu mbalimbali nchini kutoa huduma ya kiroho. Uzinduzi wa
helkopta hiyo ulifanywa na mbunge wa Monduli (CCM) na waziri mkuu wa
zamani, mheshimiwa Edward Lowassa.
Magari ya wachungaji.
ANAONGOZA KWA KUWA NA WAUMINI WENGI
Uchunguzi
pia ulibaini kwamba, Kanisa la Mchungaji Gwajima linaongoza kwa kuwa na
waumini wengi ambapo wanakadiriwa kufikia 70, 000. Kwa maana hiyo sasa,
kama waumini wake watatoa sadaka ya Jumapili kila mmoja kwa shilingi
elfu mbili, atakuwa anaingiza shilingi milioni 140 kwa ibada moja.Kwa
mwezi, Gwajima atakuwa anaingiza shilingi milioni 560 japokuwa wapo
waumini inadaiwa hutoa hadi shilingi laki tano (500,000) kama sadaka kwa
ibada moja.
MSAMAHA WA KODI
KWA
mujibu wa sheria za nchi, baadhi ya taasisi zimepewa msamaha wa kodi
wakati wa kuingiza bidhaa mbalimbali nchini, hasa zinazohusu huduma kwa
jamii. Bidhaa hizo ni pamoja na magari (Tax Exemption).
Taasisi hizo ni pamoja na za dini, elimu, afya (madaktari) na nyingine zenye kuhudumia jamii.
Magari ya kubebea waumini.
“Kwa hiyo Gwajima anaweza kumiliki mali nyingi kwa sababu anao msamaha
wa kodi, anaweza kuingiza magari mengi kwa kodi ndogo sana,” alisema
mmoja wa waumini wa Kanisa la Gwajima.
MKEWE ANASEMAJE?
Kwa
mujibu wa mke wa Gwajima, Grace alipozungumza na vyombo vya habari hivi
karibuni, alisema suala la mumewe kuzimia waulizwe polisi.“Mume wangu
aliondoka mzima kabisa, polisi ndiyo waulizwe kwa nini alizim
No comments:
Post a Comment