Sunday, April 5, 2015

HAYA NDIO MASWALI YALIYO MZIMISHA GWAJIMA KITUONI


YAFAHAMU MASWALI YALIYOMLAZA CHALI MCHUNGAJI GWAJIMA
(1) NDUGU GWAJIMA UNAWEZA KUTUELEZA UHALALI WA UTANZANIA WAKO?
(2) NDUGU GWAJIMA UNAWEZA KUTUELEZA KIPI CHANZO KIKUBWA CHA UTAJIRI WAKO UNAOFIKIA SHILINGI BILIONI 250 ZA KITANZANIA?
(3) NDUGU GWAJIMA ZAIDI YA UCHUNGAJI KAZI IPI NYINGINE UNAJIHUSISHA NAYO?
(4) TUNAHITAJI KUFANYA UPEKUZI KWENYE NYUMBA YAKO, AKAUNTI ZAKO NA TAASISI ZAKO MBALIMBALI AMBAZO UNAZIONGOZA...
HAPO HAPO GWAJIMA CHALI, YALE MAKEKE AMBAYO ALIINGIA NAYO AKIWA ANAHOJIWA NA WAANDISHI WA HABARI YALIISHIA HAPO HAPO
AKILI YA GWAJIMA,
ALIFIKIRIA ATAULIZWA KWELI AMETOA LUGHA CHAFU KWA CARDINAL PENGO, 
LAKINI PIA ALIFIKIRI ATAULIZWA KWANINI ALITOA LUGHA CHAFU KWA KIONGOZI MWENZAKE WA KANISA...
MBINU ZILIZOTUMIKA KUMCHANGANYA GWAJIMA....
ALIULIZWA JINA LAKO NANI KAMA MARA ISHIRINI HIVI,
WALIINGIA WATAALAMU TOFAUTI TOFAUTI KWA NYAKATI TOFAUTI KUMUHOJI KUTOKA VITENGO MBALIMBALI VYA UCHUNGUZI

Katika video na sauti zilizosambaa kwenye mitandao ya kijamii hasa What’s App, Gwajima alirekodiwa akiwa kwenye ibada ya kanisa lake akitumia lugha zisizokuwa na staa kwa Kardinali Pengo akimtuhumu kuwa ni msaliti kwani amekwenda kinyume na Taasisi ya Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Baraza la Makanisa ya Kipentekoste (CPCT) na Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT) kwa kuwataka waumini waisome Katiba Inayopendekezwa kisha wapewe uhuru wa kupiga kura ya “ndiyo” au “hapana” tofauti na vyombo hivyo vyenye dhamana ya kuongoza dini ya Kikristo vilivyotaka waumini waipigie kura ya “hapana”.


Dhambi zamtafuna Josephat Gwajima azimia katika kituo cha polisi ujanja wote mfukoni...

GWAJIMA NA MATUMIZI MABAYA YA UHURU WA MAONI
. katiba ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 chini ya ibara 18{a} imetoa uhuru wa mtu kutoa maoni yake hadharani"kila mtu anao uhuru wa kuwa na maoni na kueleza fikra zake"lakini katiba hiyo hiyo chini ya ibara ya 30{1}imeweka mipaka ya uhuru wa maoni kwamba mtu asitumie vibaya uhuru huo kuingilia na uhuru wa watu wengine"Haki na uhuru wa binaadamu ambavyo misingi yake imeorodheshwa katika katiba hii havitatumiwa na mtu mmoja kwa maana ambayo itasababisha kuingiliwa kati au kukatizwa kwa haki na uhuru wa watu wengine au maslahi ya umma" 
kwa hiyo askofu Gwajima ima kwa kutokujua au kwa makusudi ametumia vibaya uhuru huu wa kutoa maoni kwa kuongea uongo kwa lengo la kuvuruga amani lakini pia kumchafua kadinari pengo ambaye ni kiongozi mkubwa wa kanisa kubwa kuliko makanisa yote duniani. 
Lakini mimi kwa mtazamo wangu GWAJIMA alijua anachokifanya kwahiyo akaamua kufanya makusudi kwa kuwa yeye ni mtu muelewa anayeongozwa na roho mtakatifu na ameaminiwa kwa kuongoza maelfu ya wakristo wa kanisa la ufufuo na uzima. 

UWONGO WA GWAJIMA WENYE LENGO LA KUVURUGA AMANI
Askofu Gwajkima katika video ilioyorushwa kwanza ameanza kuitisha serikali kwauitaka isithubutu kuruhusu kuwepo kwa mahakama ya kadhi nchini,akadai kuwa iwapo muislam anpelekwa kuhukumiwa lakini njiani akakutana na muinjilisti akampa neno la mungu kisha akaokoka!{ritadi}akakataa kuhukumiwa na mahakama ya kadhi na wakristo wakamuunga mkono na iwapo waislam wakiendelea kutaka ahukumiwe na mahakama ya kadhi kutatokea machafuko. 

Gwajima katika kipengele hiki ameuongopea uma kwa sababu mahakama ya kadhi haihusiki na mambo ya jinai lakini pia hata kama ingekuwa inahusika na masuala ya jinai,kuokoka sio kinga ya mtu aliyekutwa na hatia ya kosa fulani na mahakama kutokuhukumiwa kwa kosa husika kwasababu wakati huyo mtuhumiwa anfanya kosa alikuwa ni muislam lazima aadhibiwe kwa mujibu wa hukumu ya kiislam ila atakapofanya kosa baada ya kuokoka ndio sheria za uislam hazitomuhusu kwa kuwa tyari ameshatoka katika uislam. 
kwa mfano mtu kama ameiba alafu mahakama ikamkuta na hatia ya kosa husika,hatoiachwa kuadhibiwa kwasababu tu eti kabla ya hukumu ya kosa husika ameamua kuokoka.sasa tuchukulie kwamba mfano wa Gwajima ulihusu jambo lisilo la jinai linalostahili kuhukumiwa na mahakama ya kadhi mfano wa mirathi.kama mahakama ya kadhi ilihukumu kwa huyo aliyebadili dini kwa mujibu wa uislam kuokoka kwake hakutobatilisha hukumu hiyo kwa kuwa wakati anahukumiwa alikuwa ni muislam ila akifanya jambo baada ya kuokoka ndio mahakama ya kadhi haitokuwa na mamlaka ya kumuhukumu kwa kuwa tayari amesha uacha uislam. 
utaratibu wa kisheria ni kwamba mtu hawezi kuadhibiwa kwa jambo ambalo wakati analifanya halikuwa ni kosa,kwa mfano leo hii serikali ikitunga sheria ya kupiga marufuku utengenezaji na uuzwaji wa sigara basi haiwezekani kwa viwanda vilivyokuwa vinatengeneza sigara kabla ya sheria hii kushtakiwa,kwa kuwa wakati wanatengeneza sigara ilikuwa ni halali.hivyo hivyo kama mtu alifanya kosa sheria itachukua mkondo wake hata kama ataamua kuokoka. 

GWAJIMA KUMDHALILISHA ASKOFU PENGO
Askofu Gwajima pia ametumia vibaya uhuru wa maoni kwa kutamka mamneno yenye lengo la kumdhalilisha na mkumshushia heshima askofu mwenzie kadinari PENGO. katika sheria mtu anapotamka maneno yenye lengo la kumdhalilisha mtu mbele ya watu wengim\ne ni kosa la madai linaitwa "DEFAMATION"kwahiyo ukitazama hile video ya GWAJIMA utaona namna maneno ya askofu huyo yalivyokuwa na nia ya kumfanya askofu pengo achukiwe na jamii.katika maneno yake Gwajima ametamka kuwa askofu pengo nimpuuzi,mjinga,hana akili na pia akatoa wito kwa wakristo wote kumchukia na mwisho akamuombea apate pigo.matokeo yake laana alizpmuombea PENGO zimemrudia mwenyewe kwa kuwa PENGO hakuwa na ubaya naye na hakutamka maneno mabaya bali aliwashauri tu maaskofu wenzie wasiwaamulie waumini wao juu ya kura wanazotakiwa kupiga kuhusu katiba inayopendekezwa. 

kwahiyo mimi binafsi nimefurahioshwa na serikali kwa kutumia jeshi la polisi kumwita na kumuhoji askofu GWAJIMA kutokana na maneno yake ya uchochezi na yaliyokuwa na lengo la kuchafua amani nchini kwa kuwa hilo ni miongoni mwa kazi za jeshi la polisi kusimamia utiifu wa sheria kwa raia wote kwani hakuna aliye juu ya sheria. 
Matokeo yake kutokana na sifa za kijinga alizokuwa anazitafuta kaulizwa maswali magumu mwisho anaumwa hoi,nakuomba mwenyezi mungu mponeshe GWAJIMA ili polisi iendelee na taratibu za kiuchunguzi dhidi yake na iwapo ikionekana ana kesi ya kujibu wampandishe mahakamani ili iwe fundisho kwa maaskofu wengine wanaodhani kuwa kwao maaskofu wapo juu ya sheria na wana haki ya kusema watakacho na kutokuchukuliwa hatua za kisheria.mungu ibariki Tanzania mungu mbariki Rais Kikwete na serikali yake

No comments:

Post a Comment