WALICHO KIFANYA ACT WAZALENDO HUKO URAMBO KAMWE HAKIWEZI KUSAHAULIKA NA SAMWELI SITTA,SOMA HAPA
CHama
cha ACT-Wazalendo kimeviliza vyama vinavyoundwa na Umoja wa Katiba ya
Wananchi (Ukawa) na Chama Cha Mapinduzi (CCM), baada ya mamia ya
wananchi wa Wilaya ya Urambo kutangaza kujiunga na chama hicho.
Wilaya ya Urambo ina jimbo moja la uchaguzi la Urambo Mashariki ambalo linaongozwa na Waziri wa Uchukuzi, Samuel Sitta (CCM).
Nia hiyo ya wana-Urambo ilimfanya Kiongozi Mkuu wa ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe kujikuta akibubujikwa na
machozi ya furaha, huku kila mara akiwashukuru wananchi wa Tabora kwa kumfuta machozi kwa kukubali kuwa wazalendo.
Tukio hilo la aina yake lilitokea jana mchana baada ya viongozi wa chama hicho wakiongozwa na Mwenyekiti wake, Anna Mghwira na Zitto kuzungumza katika mkutano wa hadhara uliohudhuriwa na mamia ya wananchi wa Wilaya ya Urambo.
Katika mkutano huo uliofanyika katika Uwanja wa Tarafani wilayani hapa na baadae Tabora mjini, Zitto alisema uamuzi wake wa kujiunga na chama hicho ulitokana na kuhusishwa na vitendo vya manyanyaso na kunyanyapaliwa na watu wasiomtakia mema katika chama chake cha awali.
“Ndugu zangu leo mmenifariji sina la kusema, nabaki nalia kwa machozi ya furaha, ninajua Urambo na Tabora ni mkoa wa kihistoria kuanzia kwa Mtemi Mirambo, Isike ambao walisimama imara kumwondoa mkoloni.
No comments:
Post a Comment