Naibu Spika, Job Ndugai, amesema madai yanayotolewa kuwa amezuiliwa kuendesha shughuli za Bunge ni mambo ya kawaida.
Tangu
kumalizika kwa mkutano wa Bunge wa 16 na 17 ambao ulijadili kashfa ya
uchotaji wa zaidi ya Sh. bilioni 300 katika akaunti ya Tegeta Escrow
iliyokuwa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) na Bunge kutoka na maazimio nane,
Ndugai hajawahi kuonekana bungeni kuongoza shughuli za Bunge.
Hakuhudhruia
Mkutano wa 19 na wa 20 unaoendelea hivi sasa., hali iliyozua madai
kutoka kwa baadhi ya wabunge na watu wengine kuwa amezuiliwa kuendesha
shughuli za Bunge kutokana na msimamo wake wa kuruhusu kujadiliwa kwa
kashfa hiyo bungeni.
Baadhi
ya watu ambao wamezungumza na NIPASHE kwa nyakati tofauti mjini Dodoma
walisema kitendo cha Ndugai kutoa uhuru zaidi wakati wa mjadala wa
sakata la Escrow inadaiwa hakikuwafurahisha wakubwa kwani ilipelekea
serikali kutikisika.
Ndugai
alipoulizwa na NIPASHE jana kwa njia ya simu kuhusiana na taarifa hizo,
hakuwa tayari kulizungumzia suala hilo zaidi ya kuomba asilizungumzie.
Hata
hivyo, alisema kwa kifupi: “Naomba uwaambie waachane na hiyo issue
(jambo), siwezi kuzungumza lolote, mbona ni la kawaida tu.”
Alipoulizwa kuwa kwa sasa yuko wapi, alisema kuwa alikuwa safarini bila kueleza alikokuwa akielekea.
Mbunge
wa Korogwe Vijijini (CCM), Stephen Ngonyani, alipoulizwa kama anafahamu
aliko Ndugai, alisema hafahamu kwa kuwa wabunge hawajajulishwa na ofisi
ya Bunge.
Kwa
upande wake Mbunge wa Mhambwe, Felix Mkosamali (NCCR-Mageuzi), alisema
kiutaratibu Spika wa Bunge, Anne Makinda alitakiwa kuwafahamisha aliko
Ndugai lakini kwa bahati mbaya hajatujulisha.
Taarifa za awali kutoka kwa wafanyakazi wengine Bungeni walisema Ndugai ni mgonjwa.
Wafanyakazi
hao walisema mara baada ya kikao cha Bunge cha mwezi Novemba mwaka jana
Ndugai ambaye ni pia ni Mbunge wa Kongwa, alianza kujisikia vibaya
kiafya na hivyo kwenda nchini India kwa matibabu.
Inadaiwa
Ndugai ambaye amekaa huko kwa muda mrefu alirejea nchini mwanzo mwa
wiki iliyopita na alipitia Dar es Salaam kwa ajili ya kupumzika.
Mwandishi
wa NIPASHE alipofika ofisi ya Naibu Spika kuomba kuonana naye, Katibu
Muhtasi ambaye jina lake halikufahamika, alisema Ndugai hayupo kwa muda
mrefu na hawafahamu aliko.
Chanzo
kingine kilieleza kuwa muda mfupi kabla ya Mkutano wa sasa wa Bunge
kuanza, Ndugai alikuwa Dar es Salaam akijiandaa na safari ya kwenda nje
kwa matibabu.
Hata hivyo, Katibu wa Bunge, Dk. Thomas Kashillilah, alisema Ndugai ataongoza vikao vya Bunge kuanzia leo.
Dk.
Kashililah alisema Ndugai alikuwa amesafiri kikazi nchini Ubelgiji
ambako alihudhuria mkutano na alipitia India kufanyiwa uchunguzi wa afya
yake, lakini amesharejea nchini.
Katika
kipindi ambacho Ndugai hakuwapo, vikao vya Bunge vilikuwa vinaendeswa
na Spika Makinda, wenyeviti wa Bunge, Mussa Zungu na Rediana Mng'ong'o.
“Leo
Mheshimiwa Ndugai atakuwapo bungeni kwa sababu Spika amebaki pekee yake
baada ya Mheshimiwa Zungu kwenda Dar es Salaam kwenye mafuriko na
Mheshimiwa Mng’ong’o amekwenda nje ya nchi kuhudhuria mkutano,”
alisema.
No comments:
Post a Comment