Saturday, April 18, 2015

MSANII MKUBWA BONGO ATOA USHUHUDA MZITO WA AIBU,SIKILIZA ALIKUWA ANAFANYA NINI?..IPO HAPA

Hamida Hassan
Staa wa filamu Bongo, Lungi Maulanga hivi karibuni ametoa ushuhuda wake kwamba alikuwa akisumbuliwa na tatizo la kujisaidia kitandani mpaka alipofika kidato cha pili lakini alipona katika mazingira ya kushangaza.
 
Staa wa filamu Bongo, Lungi Maulanga.
Akizu-ngumza  na Ijumaa Lungi alifunguka: “Nikiri tu kwamba nilikuwa kikojozi mpaka nafikia form two, nilikuwa naona aibu sana lakini aliyenisaida ni bibi mmoja ambaye aliniponya katika mazingira ya kushangaza.“Baada ya kumwambia tatizo langu, aliniambia nipande kwenye mti wa muembe nikiwa na nguo zangu, nikiwa juu akaniambia nikojoe kisha nishuke.
“Niliposhuka, akaniambia nibadili nguo na kusema tatizo langu limeisha, sikuamini lakini ukweli ni kwamba kuanzia siku hiyo sikujisaidia tena kitandani.”

No comments:

Post a Comment