MDOGO WAKE WA MWISHO JK,ATAKA UBUNGE!!.SOMA HAPA
Bagamoyo. Makada
wawili wa CCM wilayani Bagamoyo, wameonyesha nia ya kuingia kwenye
kinyang’anyiro cha ubunge katika jimbo hilo kupambana na mbunge wa sasa,
Dk Shukuru Kawambwa.
Makada
hao ni Mwenyekiti wa CCM kata ya Dunda, Yusufu Mrisho Kikwete ambaye ni
kitinda mimba wa familia ya Rais Jakaya Kikwete na Abdursharrif Zahoro
ambaye ni mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi CCM wilayani humo.
Wakati
makada hao wakitangaza nia hiyo juzi, tayari mbunge wa jimbo hilo Dk
Shukuru Kawambwa alikwisha tangaza nia ya kutaka kutetea nafasi hiyo
katika Uchaguzi Mkuu ujao.
Tambo za wapinzani wa Kawambwa
Abdulsharrif
alisema ameamua kuingia katika kinyanganyiro hicho baada ya makundi
mbalimbali ya wakazi wa wilaya hiyo, wakiwemo kina mama na vijana
kumuomba achukue fomu ili aweze kuwania nafasi hiyo.
“Nimefuatwa
sana jamani na wananchi wa hapa, wakati mwingine hadi naona aibu
kujificha maana nahisi ni Mungu amewaonyesha kiongozi anayewafaa safari
ijao, kwa hiyo nimekubaliana na maombi hayo, nitajitokeza kukabiliana na
Dk Kawambwa,” alisema.
Naye
Yusuph Kikwete alisema ana matumaini makubwa ya kushinda kwa kuwa,
amekuwa akiungwa mkono na makundi mbalimbali, wakiwamo vijana ambao
wamekuwa wakimshawishi kugombea nafasi hiyo.
“Ni
kweli kuna makundi mengi, yamekuwa yakinishawishi kuingia katika
kinyang’anyiro na baada ya kutafakari sana na kujipima kama ilivyo kwa
wanasiasa wengine, nimeona siwezi kukataa ushawishi huo, maana kuna watu
wameona uwezo wangu wa kiuongozi,” alisema.
Mapema
wiki hii Dk Kawambwa aliweka wazi kuwa anaingia tena katika
kinyang’anyiro hicho kutokana na kuridhishwa na mambo mbalimbali
aliyofanya kwa wapigakura wa jimbo hilo.
“Ninarudi
na wana Bagamoyo wameniomba nifanye hivyo kutokana na kufanya mengi ya
maendeleo, mfano katika kipindi changu cha miaka kumi, nimeweza
kushughulikia changamoto kubwa zilizokuwa zikiwakabili wakazi wa jimbo
hili, ikiwamo masuala ya elimu, afya na maji.
No comments:
Post a Comment