Monday, April 6, 2015

KHANGA MOKO ANUSURIKA KUBAKWA CHOONI..SOMA HAPA

 
KAMA kawa kama dawa, ni Ijumaa nyingine ambayo mapaparazi wetu wanaotii amri za Mkuu wao walijiachia viwanja mbalimbali kusaka matukio na kuwasiliana moja kwa moja na Mkuu wao aliyekuwa makao makuu ya ofisi za gazeti hili zilizopo Bamaga Mwenge jijini Dar es Salaam. Kikosi cha mapaparazi hao ni Musa Mateja ‘Toz’, Issa Mnally ‘Mzee wa GX100’, Dustan Shekidele ‘Mkude Simba’ na Mpigapicha Mkuu, Richard Bukos.
Saa 12:56 jioni
Makao Makuu: Mkuu akiwa ofisini anaanza kumtwangia Musa Mateja ‘Toz’ aliyekuwa mitaa ya Tandale kwenye tamasha kubwa la ujasiriamali ambalo amini usiamini linatarajiwa kuwafanya wakazi wa mitaa hiyo kuwa mabilionea. 
 

WATOTO WA TANDALE WAMTAITI YOUNG KILLER AWAIMBIE AKAPERA
Makao Makuu: Mateja umeshafika Tandale kwenye tamasha la ujasiriamali?
Mateja: Ndiyo Mkuu nipo hapa ila bahati mbaya leo ni Ijumaa Kuu, hivyo naona kama tamasha linataka kukatishwa kwa ajili ya kuwapisha watu kwa ajili ya ibada.
Makao Makuu: Duuh! Sasa itakuwaje kwa hao wasanii waliotakiwa kutumbuiza hapo?
Mateja: Mimi mwenyewe nashindwa kutambua ila hadi sasa Masanja Mkandamizaji ndiyo yupo hapa na ameshawekwa mtu kati na watoto wa Tandale wanamuomba kupiga naye picha na wengi wanamshangaa tu.
Makao Makuu: Oooh, basi komaa nao, ukiachana na Masanja staa gani mwingine yupo hapo?
Mateja: Mkuu hivi tunavyoongea mkurugenzi wetu, Eric Shigongo anaendelea kuongea na baadhi ya watu waliofika hapa kabla ya kutangaziwa kuahirishwa kwa hili tamasha.
Makao Makuu: Aaah, ‘baunsa’ wake, Nyange leo inaonekana kapata kazi kubwa sana, maana kila mtu nafikiri atakuwa anatamani kumshika mkono Shigongo.
Mateja: Hilo ni kweli kabisa bosi yaani kama ulikuwepo. Kingine msanii wa muziki wa kizazi kipya, Young Killer kafika hapa sasa kuna jamaa wamemganda wanataka awaimbie japo akapela kidogo.
Makao Makuu: Haaa! Huyo kazi anayo. Basi sawa kijana wangu wewe malizana nao hapo ngoja nivute pumzi kidogo kisha baadaye nimcheki Mnally.
Mateja: Haya Bosi wangu.
Saa 4:56 usiku


KHANGA MOKO NUSURA ABAKWE CHOONI
Makao Makuu: Mnally upo pande zipi?
Mnally: Kiongozi mimi leo nipo ndani ya Ukumbi wa Santiago huku Msongola.
Makao Makuu: Yaah, kuna nini hapo leo?
Mnally: Mkuu huku leo kuna vibweka vya nguvu kuna shoo ya Khanga Moko na vijana wa kusheki.
Makao Makuu: Duuh! Kweli huko leo kazi ipo. Kuna lolote ulilonasa hapo?
Mnally: Ndiyo Mkuu kuna njemba moja imepata kipigo cha mbwa mwizi baada ya kumvizia chooni mnenguaji mmoja wa Khanga Moko na kutaka kumbaka baada ya kuchanganywa na mauno ya jukwaani.
Makao Makuu: Duu! Ikawaje?
Mnally: Ilibidi wasamaria wema waingilie kati baada kusikia kelele katika choo cha kike.
Makao Makuu: Hahaa! Haya Mnally endelea na kazi  ngoja nitulie kidogo kisha nimcheki Mpigapicha Mkuu, Richard Bukos nimsikie yuko pande gani.
Mnally: Sawa Mkuu.
Saa 6:12 usiku
  

MANGI MUUZA CHIPSI AMALIZANA NA CHANGU, UCHOCHORONI.
Makao Makuu: Haloo Bukos haya niambie uko wapi?
Bukos: Mkuu niko hapa Sinza, Afrika Sana nje ya Corner Bar na Ambiance Club naangalia matukio.
Makao Makuu: Kuna vituko gani hapo?
Bukos: Mkuu kuna mdada flani nahisi ni changu eti amekula mishkaki na chipsi baada ya kumaliza anamwambia muuzaji, eti hana hela kama akitaka wazunguke uchochoroni wakamalizane.
Makao Makuu: Vipi huyo muuzaji amekubali?
Bukos: Mkuu huyu muuzaji ni mangi f’lani, kaangalia kila upande alipoona hakuna watu wanaosikiliza maongezi yao naona kamkubalia kimtindo kampa ishara ya poa na ugomvi wa kudai chake umeisha.
Makao Makuu: Dah, huyo mangi mtaji wake hauwezi kufika mbali. Sawa Bukos piga kazi mimi ngoja nimcheki Dustan Shekidele ‘Mkude Simba’.
 
Saa 7: 23 usiku


HOUSE GIRL AADHIBIWA KWA KUUNGUZA SUTI YA PASAKA
Makao Makuu: Yaani wewe Mkude Simba unataka kazi hutaki kazi, kwa nini nakupigia simu robo saa nzima simu yako iko bize?
Shekidele: Samahani Mkuu nilikuwa naongea kwenye simu na house girl flani ananieleza shida zake.
Makao Makuu: Shida gani tena usiku wote huu?
Shekidele: Anasema leo jioni wakati akimpigia pasi bosi wake suti yake ya Pasaka kwa bahati mbaya ikaungua baada ya kunogewa na maongezi ya simu aliyopigiwa na bwana’ake. Sasa akaambiwa adhabu yake anakatwa mshahara wa miezi minne ambayo hajalipwa na kesho alfajiri ameambiwa arudi kwao Iringa mpaka atakapopigiwa simu ndiyo arudi.
Makao Makuu: Duh! Hiyo kali, haya endelea na kazi ukimaliza wapigie simu wenzako mkapumzike.

No comments:

Post a Comment