JK AANIKA MAGUMU KATIKA UTAWALA WAKE!!
Dar es Salaam.
Wakati makada wa CCM wakipigana vikumbo kuwania kupitishwa na chama chao
kuwania urais, Rais Jakaya Kikwete anayemaliza ngwe yake amesema nafasi
hiyo ni kadhia, ni kazi ngumu na si ya kukimbilia.
Rais Kikwete
aliyasema hayo juzi nchini Marekani, wakati akihutubia kwenye taasisi
inayoitwa, Woodrow Wilson International Center for Scholars, ambapo
alitumia muda huo kuelezea mafanikio na changamoto katika kipindi chake
cha miaka 10 ya uongozi wake.
“Wakati unaingia
Ikulu unakuwa na shauku kubwa sana pamoja na furaha ya ushindi, lakini
kwa hakika urais ni kadhia kubwa, ukipata fursa ya kuwa rais kwa awamu
mbili kama mimi, nadhani zinatosha kabisa, nimefanya mengi kwa nchi
yangu, atakayekuja ataendeleza nilipoishia,” alisema Rais Kikwete.
Alitumia fursa
hiyo kuieleza dunia kwamba baada ya kustaafu nafasi yake Oktoba baada ya
Uchaguzi Mkuu, atatumia muda wake mwingi kujihusisha na kilimo, lakini
anajipanga pia kuanzisha taasisi itakayojishughulisha na masuala ya vifo
vinavyotokana na uzazi pamoja na malaria.
Alisema
akitazama nyuma mwaka 2005 alipokuwa anaingia Ikulu, hana cha kujutia
mpaka sasa anapojiandaa kuondoka Ikulu ya Magogoni, ila anasema
amejifunza mambo mengi.
“Ninaamini
kwamba mrithi wangu ataendeleza pale nilipoishia, ninachoweza kujivunia
ni kwamba tumeweza kujenga misingi imara katika kulielekeza Taifa letu
kwenye Dira ya Maendeleo 2025, ambayo imejikita katika kuifanya nchi
yetu kuwa ya uchumi wa kati,” alisema Rais Kikwete.
Aliongeza,
“Ninadhani nitaweza kuacha sera madhubuti ya masuala ya uchumi wa gesi
pamoja na mapato ambayo matunda yake yataanza kuonekana 2020. Bila shaka
tutakuwa na uchaguzi huru, haki na kwamba ninaisubiri kwa hamu siku ya
kuikabidhi Ikulu kwa rais ajaye,”
Utengamano wa kitaifa
Akijibu swali la
mwongoza mjadala, Monde Muyangwa kuhusu ni namna gani amefanikisha
kuliweka Taifa pamoja mbali na changamoto zilizopo duniani kote, Rais
Kikwete alisema ni kutokana na misingi ambayo imeachwa na waasisi wa
Taifa, Mwalimu Julius Nyerere na Sheikh Abeid Karume.
“Katika kipindi
changu kumekuwa na changamoto za kutaka kutumia madhehebu ya dini
kisiasa, nimekuwa mstari wa mbele kukemea matukio hayo.
“Nimekuwa
natumia muda wangu kukutana na viongozi wa dini kuwakumbusha umuhimu wa
amani tuliyonayo pamoja na dhamana wanayobeba katika jamii,” alisema
Kikwete. Alisema Tanzania ni nchi ambayo ina makabila takriban 120,
pamoja na rangi mbalimbali na Watanzania wengi ni wafuasi wa dini na
baadhi wakiwa hawana dini na pengine bado hawajaamua kuchagua, lakini
wote wanaishi pamoja.
Alisema baada ya
kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi mwaka 1992, kulianza kuwa na dalili
za kutofautiana kimtazamo kitu ambacho kingeweza kutarisha Amani na
mshikamano wa Taifa
No comments:
Post a Comment