Kikao cha Bunge kimevunjika muda mfupi uliopita baada ya kutokea vurugu za maneno kufuatia wapinzani kutaka Waziri Mkuu atoe taarifa juu ya mwenendo wa kura ya maoni ya katiba mpya april 30,2015.
Kutokana na vurugu hizo za dakika kama 10 hivi Spika Anna Makinda amesitisha gafla shughuli za bunge hadi mchana.
Hali likuwa hivi:
Mnyika: Nimesimama
kupata idhini kwa mujibu wa kanuni ili shughuli za bunge zisitishwe
badala yake tujadili zoezi la uandikishaji nchi nzima.
Mpaka
sasa zoezi halijakamilika hata kwa mkoa mmoja tu wa Njombe, jambo hili
ni la dharura na lilishatolewa na ukaagiza kamati ishughulikie.Tunaomba
majibu tupate kikao hiki na leo tunafunga mkutano.
Spika Makinda: Hoja
hii inafanana na ile ya kwanza( Hoja ya mbunge wa Kisarawe Seleman
Jafo ambaye alipendekeza kura ya maoni ya katiba inayopendekezwa
isogezwe mbele na badala yake kuwe na katiba ya mpito kuelekea
uchaguzi mkuu)
Baada
ya kauli hiyo, Mnyika na wabunge wa upinzani walianza kupiga
kelele bungeni wakidai kuonewa huku wakimtuhumu Spika makinda
kuibeba serikali.
Hata
hivyo, Spika hakuonesha kutishwa na kelele hizo na badala yake
alimtaka katibu wa Bunge atoe mwongozo wa kile kinachofuata.
Katibu
alisimama na kuanza kusoma miswada ya habari ambapo wapinzani
nao walisimama na kuzidisha kelele huku wakisema:"Tunataka majibu..Tunataka majibu. Tumechoka kuburuzwa..Makinda kwanini unailinda Serikali.??!!!
Tazama Video hapo chini
No comments:
Post a Comment