Takriban miaka mitatu imekatika tangu kifo cha aliyekuwa staa wa
Bongo Movies, Steven Kanumba huku watu wawili wakifariki dunia kwa
nyakati tofauti lakini nyuma ya pazia ya vifo vyao, mzimu wa Kanumba
unatajwa kuhusika kutokana na watu hao kutaka kuishi mahali pa marehemu
huyo, gazeti la Risasi limeripoti.
Itakumbukwa kwamba, baada ya kifo cha Kanumba, mama yake mzazi, Flora
Mtegoa ndiye aliyeshika jukumu la kusimamia mali za marehemu mtoto wake
(alikuwa na haki).
Miongoni mwa mali hizo ukiachilia mbali, magari, vifaa vya kurekodia
filamu, viwanja na filamu zilizokuwa hazijalipwa, mama Kanumba
aliimiliki ofisi ya Kanumba iliyokuwa ikijulikana kwa jina la Kanumba
The Great Film iliyokuwa Sinza.Hata hivyo, hivi mapema Februari, mwaka
huu, mama Kanumba alitoa vitu kwenye ofisi hiyo kwa madai ya kushindwa
kulipa pango, hivyo ofisi ikawa wazi.
Habari ambazo zimeandikwa na gazeti hilo zilidai kwamba, mpangaji
mwingine aliikodisha ofisi hiyo kwa mkataba wa mwaka mmoja lakini hivi
karibuni mtu huyo amefariki dunia.Msikilize shuhuda: “Kuna jamaa
alipanga kwenye ofisi iliyokuwa ya Kanumba mara tu baada ya mama Kanumba
kuondoka vitu kwa kushindwa kulipia mkataba mpya.
“Huyo jamaa alikuwa anahusika na masuala ya ujenzi. Jamaa alilipia
kodi ya mwaka mmoja, akawalipa watu wamfanyie usafi yeye akaenda ‘saiti’
kwenye mambo yake ya ujenzi. Inadaiwa akiwa kule, kuna ‘kijiko’
kilichokuwa kinachimba kiwanja, bahati mbaya kikarudi nyuma na kumgonga,
akaanguka na kufariki dunia.”
Kifo cha mtu huyo ambaye jina lake halikuweza kupatikana mara moja,
kinaunganishwa na tukio lilitokea mwaka juzi baada ya kifo cha Kanumba
kilichotokea Aprili 7, mwaka 2012.Mara baada ya Kanumba kufariki dunia
ghafla, mwanamke mmoja alikwenda kupanga nyumba ile aliyokuwa akiishi
marehemu iliyopo Sinza, Dar, naye alifariki dunia ghafla.
Wakati wa tukio hilo, wanahabari wa gazeti hilo walifika nyumbani kwa
mwigizaji huyo ambapo walizungumza na majirani wakaelezea juu ya uwepo
wa tukio hilo.Walisema japo hawaamini juu ya imani za masuala ya mzimu
wa marehemu lakini kitendo cha mwanamke huyo kufariki dunia muda mfupi
baada ya Kanumba kufa kiliwafanya washtuke na kuamini kwamba huenda ni
mzimu wa Kanumba ndiyo ulichukua roho ya mpangaji huyo.
Hata hivyo, baadhi ya watu wengine pia walisema yao wakidai kwamba,
wanaamini kifo cha mwanamke huyo ni cha kawaida kama ilivyo kwa vifo
vingine.“Kama siku za Kanumba zilivyokuwa zimewadia na huyo mpangaji pia
siku zake zilikuwa zimefika ndiyo maana amefariki dunia,” alisema mmoja
wa majirani.
Mzee mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Mohamed Sumali (76), mkazi wa
Mabibo-Relini, Dar akizungumza na gazeti hili kuhusu mazingira ya vifo
hivyo, alisema:“Ipo mizimu ya hivyo. Mtu akifa, wa kwanza kuhamia kwenye
nyumba aliyokuwa akiishi marehemu naye anakufa. Lakini si kwamba nyumba
ndiyo ina mizimu. Kama hivyo vifo vimetokea kweli basi na mzimu wa
Kanumba umeshaondoka.”
Baada ya kuzipata habari hizo, mwanahabari wa gazeti hilo alimvutia waya
mama Kanumba kutaka kujua kama anajua lolote juu ya marehemu mtoto wake
kuacha mzimu ambao unahusishwa na vifo hivyo ambapo alikiri kusikia
taarifa za kifo cha jamaa aliyepanga kwenye ofisi za Kanumba lakini
akasema hata yeye hajui sababu za kifo chake.
“Hata mimi nimesikia, lakini sielewi chochote kuhusiana na mtu huyo
kufariki dunia. Imenishtua kwa kweli maana si unakumbuka hata kule
alikopanga (Kanumba) mwanzoni nako aliyepanga ile nyumba naye alifariki?
Sijui hata ni kwa nini?” alihoji mama Kanumba kwa sauti iliyoashiria
kushangaa sana.
No comments:
Post a Comment